Taasisi India kutoa mafunzo huduma za afya

Tanzania imepanga kushirikiana na Taasisi ya Global Health Foundation ya nchini India katika mafunzo ya wataalam na utoaji wa huduma za afya kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, jana Julai 30, 2023 alipotembelea taasisi hiyo iliyopo Hyderabad nchini India huku akiipongeza taasisi hiyo kwa ubunifu na uvumbuzi wa teknolojia mbalimbali zinazochangia mapinduzi makubwa ya utoaji wa huduma za afya duniani kote ikiwemo Tanzania.

Kwa upande wake mwanzilishi wa taasisi hiyo, Dk Ravindrapath Kancharla ameeleza kuwa, taasisi yake imeanzisha Chuo Kikuu cha Afya, Sayansi na Teknolojia ( Global Health – Tech Life Sciences University and Innovation Hub) kwa lengo la kujikita zaidi katika utoaji wa mafunzo, utafiti na ugunduzi wa teknolojia mbalimbali kusaidia utoaji wa huduma bora za Afya.

Advertisement

“Tumegundua teknolojia inayosaidia kujua kama mgonjwa amefanyiwa huduma za dialysis ipasavyo, pia tumegundua kifaa kinachowasaidia watoto wenye usonji (Autism) kujifunza kuongea ambapo kifaa hicho kina uwezo wa kutumia lugha mbalimbali ulimwenguni ikiwemo kiswahili” amesema Dk Ravindrapath Kancharla.

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *