Tama, UNFPA, kutoa mafunzo ya ukunga

CHAMA Cha Wakunga Tanzania (TAMA) kwa kushirikiana na serikali ,UNFPA na Chama cha Wakunga Canada wameanda mafunzo maalumu ya wakunga kwa wamama wanaojifungua ya mradi wa thamini uzazi salama yenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye kutoa huduma za dharura kwenye vituo vyao.

Mafunzo hayo yatafanyika Dar es Salaam siku tano kwa kundi la kwanza ambapo yana wakunga 30 huku kundi lingine la wakunga ni siku 10 zijazo ambapo jumla itakuwa siku 15 matarajio ni kuwafikia wakunga 90 wanaofanya kazi kwenye vituo vya afya vya kutolea huduma za afya kwa Mkoa wa dar es salaam.

Hayo ameyasema leo Dk.Beatrice Erastus Mwilike Rais wa Chama cha Wakunga Tanzanua (TAMA) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo na kusema kuwa changamoto kubwa wanayokabiliana nayo wamama kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua hivyo mafunzo hayo yatamjengea mkunga kukabiliana na changamoto hiyo.

Advertisement

“Mafunzo hayo tunaangalia je wakunga wanaweza vipi kumsaidia mama anayepoteta damu kipindi ambacho ni mjamzito kabla hajajifungua ,pia tunatoa mafunzo kwenye kuangalia ni namna gani wakati wa uzazi pengine mama anataka kujifungua mabega yamenasa ni namna gani tutamsaidia hivyo tunawaelekeza ni namna gani ya kufanya kuweza kumsaidia lakini pia kuna ile mama ameshindwa kujifungua kawaida kuna namna yakuweza kumsaidia mama huyo hivyo mafunzo haya yote yatawasaidia wakunga hawa,” amesema Beatrice.

Agness Mgaya Mratibu wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto Dar e Salaam amesema changamoto zipo nyingi katika kuhudumia mama mjamzito pamoja na kichanga na hasa pale dharura inapokuwa inajitokeza hivyo mafunzo hayo yatasaidia kuwapa uelewa zaidi.

“Tunajua kuwa tunafanya vizuri kuwahudumia hawa wajawazito na watoto wachanga lakini lazima kila wakati tuwape watu elimu kwani kutoa huduma ya afya ni sayansi na sayansi inakuwa inabadilika kila siku kwaiyo pale ambapo panakuwa na maboresho lazima na sisi wakunga wetu wasiachwe nyuma waweze kujengewa uwezo na kukumbushwa nini ambacho kinapaswa kufanyika.

“Bado tunachangamoto kubwa sana kwenye ushiriki wa wenza kwenye huduma za afya uzazi na mtoto wanaume wamekuwa wapo mbali kuwasindikiza wake zao kwahiyo hapa nitoe wito wanaume waweze kuwasindikiza wake zao wanapoenda kupata huduma za afya ya uzazi mama anapokuwa mjamzito lakini pia wakati mama anapojifungua wamsindikize inamsaidia sana mama kupata moyo kwamba yupo na mwenzake na kumpunguzia maumivu ” amesema Agness.

Nao wakunga walioshiriki mafunzo hayo Paul Zakaria na Sarah Hallan wamesema mafunzo hayo watakayoyapata itawajengea uwezo na watatuwa kipaumbele kwa wengine pindi warudipo kwenye vituo vyao vya kazi.

Mradi huo wa mafunzo ya thamini uzazi salama ni wa miaka saba na unatekelezeka kwa mkoa wa Dar es salaam na Shinganga kwani vifo vya Mama na mtoto kwenye mikoa hiyo imeonekana ni kinara.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *