Tanroads kujiandikisha uchaguzi mitaa

WATUMISHI wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la Mpiga Kura, ili watumie haki yao kupiga kura na kuwachagua viongozi wa Serikali za Mitaa katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta ametoa kauli hiyo leo na kuwataka watumishi wa taasisi yake, ambao wapo kwenye mikoa ya Tanzania Bara kutumia fursa hiyo kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

SOMA: Laigwanani wahamasisha uchaguzi mitaa

Besta pia amehimiza kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi, ili wakachague viongozi wenye kusimamia maendeleo kama vile maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa.

“Naendelea kuhimiza kwa kuwa zimebaki siku chache basi watumishi wenzangu mhakikishe mnakwenda kujiandikisha na mwisho siku ya kupiga kura napo mkapige kura kwa kuchagua viongozi bora wenye kutuletea maendeleo katika maeneo yetu,” amesisitiza Besta.

SOMA: DC Ilala atoa elimu uchaguzi mitaa

Habari Zifananazo

Back to top button