Tanzania, Austria kuimarisha elimu, utalii

SERIKALI ya Tanzania pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Austria zimekubaliana kuimarisha sekta za elimu ya ufundi pamoja na utalii.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika mkutano wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Angelah Kairuki na Waziri wa Kazi na Uchumi wa Austria, Profesa Martin Kocher walipokutana katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam leo.

Waziri Kairuki amesema kuwa wamekubaliana kushirikiana katika masuala ya kilimo, elimu ya ufundi ambapo Tanzania kwa sasa msukumo wake ni elimu ya ufundi na tayari serikali imeanza kuboresha sera ya elimu na mitaala ya elimu.

“Austria wameonesha nia ya kushirikiana na Tanzania katika masuala ya tasnia ya ukarimu na utalii, wenzetu kwa mwaka wanapata watalii takriban milioni 40 na wamepiga hatua kubwa, nimefurahishwa pia kuona katika ujumbe alioambatana nao Profesa Kocher kuna wafanyabiashara na wawekezaji ambao wameonesha nia ya kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya utalii, uwekezaji wa hoteli na mnyororo mzima wa thamani katika sekta ya utalii amesema Kairuki.

Ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine, wamekubaliana kushirikiana katika sekta za afya, pamoja na sekta binafsi nchini kwa kuwa mazingira ya biashara na uwekezaji ni salama na rafiki.

Naye Waziri wa Kazi na Uchumi wa Austria, Profesa Kocher amesema Austria itaendeleaa kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali hususan miundombinu, kilimo, usindikaji wa chakula, elimu ya ufundi, afya, ajira/kazi, nishati pamoja na utalii kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Tanzania kufungua ubalozi wake nchini Austria, umetuwezesha kushirikiana katika sekta mbalimbali mathalan sekta ya elimu ya ufundi pamoja na utalii.” amesema Profesa Kocher.

Ameongeza kuwa asilimia 40 ya vijana nchini Austria wamekuwa wakipatiwa elimu ya ufundi katika fani tofautitofauti, hivyo Austria inaamini kuwa endapo watashirikiana na Tanzania kuwapatia vijana elimu ya ufundi itasaidia kuwawezesha kupata fani mbalimbali zitakazo wasaidia kujenga maisha yao na kuinua uchumi wa taifa kwa ujumla.

Kuhusu sekta ya utalii, Profesa Kocher amesema kuwa Austria itaendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na utalii endelevu pamoja na kuhakikisha kuwa mataifa hayo yanakuwa na vivutio bora vya utalii kwa miongo ijayo.

Pamoja na mambo mengine, mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Austria kwa manufaa ya pande zote mbili.

Waziri Kocher yupo nchini Tanzania kwa ziara yake ya kikazi ya siku moja na ameambatana na ujumbe wa wawekezaji 20 kutoka Austria wanaolenga kuwekeza nchini Tanzania katika sekta za utalii, afya, nishati, elimu, ujenzi na miundombinu

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Susanames
Susanames
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by Susanames
Royal
1 month ago

[ JOIN US ] I am making a good salary from home 16580-47065/ Doller week , which is amazing under a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions and now it’s my duty to pay it forward and share it with Everyone,
Here is I started.…………>>  http://Www.SmartCash1.com

Last edited 1 month ago by Royal
Marry
Marry
1 month ago

●Im making over $13k a month working part time. I kept hearing other people tell me how much money they can make online so I decided to look into it. Well, it was all true and has totally changed my life.(zs)last month her pay check was $12712 just working on the laptop for a few hours. This is what I do, ↓↓↓↓VISIT THIS WEBSITE↓↓↓↓
HERE☛…..☛ http://Www.Smartcareer1.com

Julia
Julia
1 month ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month I have earned and received $18,539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money online.
.
.
Detail Here—————————————————————->>>  http://Www.BizWork1.Com

Back to top button
4
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x