Tanzania, Guinea Ikweta kuimarisha diplomasia

RAIS mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewasilisha ujumbe maalumu wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Serikali ya Guinea ya Ikweta ukihamasisha kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.

Ujumbe huo umepokelewa na Waziri wa Nchi  Wizara ya Mambo ya Nje ya Guinea ya Ikweta, Simeon Oyono Esono Angue kwa niaba ya Rais wa nchi hiyo, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.

Uwasilishaji wa ujumbe huo ulifanyika katika ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje jijini Malabo Aprili 13 2025.

Katika tukio hilo, Kikwete pia alielezea juu ya shauku ya Rais Samia kuimarisha ushirikiano, mshikamano, na umoja baina ya nchi za Afrika ili kukabiliana kwa pamoja na changamoto zinazokabili Bara la Afrika na dunia.

Habari Zifananazo

3 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button