Tanzania kuwa Guangzhou

MRADI mkubwa wa  Kituo cha Biashara cha Afrika Mashariki (EACLC) unaojengwa Ubungo unatarajiwa kuwa kiunganishi kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati na ndio wadhamini wakuu wa Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’.

Hayo yamesemwa leo Julai 4, 2023 na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akizungumza leo Julai 4, 2023 katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ ikiwa ni siku ya taifa la China

Amesema, mradi huo ambao una thamani ya dola la Kimarekani milioni 81.827 utaifungua Tanzania kibiashara na kukuza uchumi kutokana na biashara zitakazokuwa zikifanyika na kukuza mahusiano ya Kimataifa kwa kuwa na muingiliano wa wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali.

‘Ni mradi mkubwa, ambao utakidhi  mahitaji ya wafanyabishara wa aina tofauti tofauti “Kutokana na ukweli huo, mtakubaliana nami kuwa kituo hiki kitapanua fursa ya Watanzania wengi kufanyabiashara katika eneo hilo.”Amesema Kigahe na kuongeza

“Tanzania itakuwa kiunganishi cha biashara kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, badala ya watu kufuata bidhaa China sasa watazifuata Tanzania.”Amesema

Kituo hicho kitatoa ajira za moja kwa moja zaidi 15,000 na utahamasisha maendeleo ya setka mbali mbali ambazo nazo zitazalisha ajira zisizo za moja kwa moja 50,000 hivyo kuongeza mapato na kuboresha hali ya maisha kwa wananchi wa Tanzania.

Mradi huo unatarajiwa kuwa na maduka 2060 yenye ukubwa wa jumla ya mita za mraba 75,000 ambapo eneo hilo litakuwa na huduma zote za kibiashara ikiwemo mabenki na huduma ufungishaji na usafirishaji.

Pia, Mapato ya jumla kwa mwaka yanatarajiwa kufikia  zaidi ya USD Milioni 500 mradi huo ukikamilika hivyo kusaidia katika ukuaji wa pato la Taifa la Tanzania na kuongeza mapato ya kikodi.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button