Tanzania mguu sawa kuanza mradi Mchuchuma,Liganga

SERIKALI imesema ipo katika hatua za mwisho za majadiliano na wawekezaji katika mradi wa chuma Liganga na makaa ya mawe Mchuchuma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema hayo alipozungumza na wahariri wa vyombo vya habari Dar es Salaam.
Profesa Kitila amesema mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na mradi wa chuma wa Liganga ni muhimu katika utekelezaji wa ajenda ya kitaifa wa ujenzi wa viwanda kama moja ya sekta za kimageuzi.
SOMA: Samia atangaza neema Mchuchuma, Liganga
Alisema kupitia rasilimali ya makaa ya mawe yaliyopo Mchuchuma serikali itapata fursa ya kuzalisha umeme megawati 600 kwa ajili ya viwanda na chuma itazalisha malighafi muhimu za viwandani.
Profesa Kitila amesema utekelezaji wa mradi wa kuzalisha na kufua chuma Liganga utaifanya Tanzania kuwa nchi ya nne kwa uzalishaji wa chuma Afrika baada ya Afrika Kusini, Misri na Libya.
Amesema mchakato wa utekelezaji wa mradi hiyo ulianza mwaka 1996 wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu ukiwa chini ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) waliopewa jukumu la kutafuta wawekezaji wa mradi huo.
Profesa Kitila amesema kampuni 48 ziliomba kuwekeza katika mradi huo na Kampuni ya Sichuan Hongda Corporation (SHG) kutoka China ilishinda zabuni hiyo.
Amesema kampuni hiyo ilisaini mkataba na NDC na kuanzisha Kampuni ya ubia ya Tanzania China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) huku NDC ikiwa inamiliki asilimia 20 na SHG ikimiliki asilimia 80.
“Mwaka 2015 utekelezaji wa mradi ulisitishwa baada ya serikali kubaini kuwa baadhi ya masharti ya mkataba wa ubia hayakuzingatia kikamilifu masilahi mapana ya nchi,” amesema Profesa Kitila.
Amesema mwaka 2017 serikali ilipitia upya mkataba ya mradi huo na kuondoa vipengele vilivyoonekana vina changamoto na mwaka 2024 Kampuni ya Shudao Investment Group Company (SDIG) iliinunua Kampuni ya SHG.
“2025 serikali imekuwa ikijadiliana na Kampuni ya SDIG kuhusu vipengele vya mkataba ambavyo serikali haikuridhika navyo, mazungumzo yapo hatua za mwisho na tumeshakubaliana mambo mengi ya msingi,” amesema Profesa Kitila.
Ameongeza: “Serikali imeshalipa fidia katika eneo la mradi na sasa linamilikiwa na serikali kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huo”.
Profesa Kitila amesema serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali imefanya mapitio ya sheria zote ili ziendane na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Tume ya Taifa ya Mipango imefanya mapitio ya sera ziendane na dira hiyo.
Amesema sheria inasema baadhi ya shughuli za ujenzi zitafanywa na kampuni za Kitanzania na ni lazima zihusike na zishiriki katika mradi huo na mradi utakapokamilika wananchi watapata ajira na kubadilisha maisha ya watu wa maeneo hayo ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika miradi mikubwa ya taifa.
Everybody can earn $250+ daily… You can earn from $19845-$38514 a month or even more if you work as a full time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity..
go to this site home tab for more detail thank you…… https://Www.Jobathome1.Com