Tanzania U17 yatinga fainali AFCON 2025

Kikosi cha Serengeti Boys kilichoanza dhidi ya Sudan Kusini leo.

TIMU ya taifa ya wavulana chini ya miaka 17(Serengeti Boys) imetinga fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON 2025) na fainali ya CECAFA kufuzu AFCON baada ya kuibamiza Sudan Kusini mabao 4-0.

Serengeti Boys imefikia hatua hiyo wakati wa mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya kufuzu AFCON kanda ya CECAFA inayofanyika kwenye uwanja wa Nakivubo uliopo mji mkuu wa Uganda, Kampala.

Tanzania U17 sasa inasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Uganda na Somalia inayopigwa baadaye leo kufahamu itacheza na timu ipi fainali ya CECACA.

Advertisement