DAR ES SALAAM: Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika usafirishaji wa kemikali mbalimbali za sumu ikiwemo ya Sianidi inayotumika kuchenjulia dhahabu migodini katika maeneo mbalimbali nchini.
Hayo yamesemwa na mkemia kutoka mamlaka hiyo, Derick Masako wakati akizungumza katika kampeni ya elimu kwa umma kuhusu kemikali hiyo kwa watu wanaoishi pembezeni mwa barabara iliyofanyika katika kituo cha dala dala Mbezi Luis, Dar es salaam ili kuchukua.
Ofisa Afya na Usalama Mahali Pa kazi kutoka Kampuni ya Usafirishaji Taifa, Bestina Kitinya amesema tangu wameanza kusafirisha kemikali hizo hakuna madhara yoyote yaliyowahi kutokea kutokana na usimamizi mzuri wanaoufanya na kwamba elimu hiyo wataifanya katika mikoa yote ambayo kemikali hiyo inapita.
Aidha watumiaji wa vyombo vingine vya moto wamehimizwa kuwa makini wanapoyapita magari hayo ilikuepuka kuyagonga.