Tanzania yapokea magari 10 ya wagonjwa

WAZIRI wa Afya,Ummy Mwalimu leo amepokea magari 10 ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya Sh bilioni . 1.1 kutoka Serikali ya India.

Waziri Ummy ameyapokea magari hayo Jijini Dar es Salaam na ameishukuru Serikali ya India kupitia kwa Balozi wa India nchini, Binaya Pradhan kwa msaada huo ambao unaendelea kuonesha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.

“Serikali ya India imekua na ushirikiano Mkubwa na Serikali ya Tanzania ikiwemo katika Sekta ya Afya, hivyo nitumie fursa hii kuwashuku sana kwa msaada wa magari haya ambayo hata kwenda kusaidia kurahisisha huduma kwa Watanzania,” amesema Ummy.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button