Tanzania yashiriki mkutano wa mazingira Denmark

COPENHAGEN : UBALOZI wa Tanzania nchini Sweden umeratibu ushiriki wa ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira duniani unaofanyika tarehe kuanzia leo tarehe 7 hadi 8 Mei, 2025, jijini Copenhagen nchini Denmark.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Masauni, ambapo mawaziri 30 wanaosimamia masuala ya mazingira kutoka katika mataifa mbalimbali, Kamisheni ya Umoja ya Ulaya na wadau wengine wa mazingira wameshiriki.

Lengo la mkutano huo ni kupokea taarifa ya kila nchi ya namna ilivyochangia katika kupunguza gesi joto duniani, kubadilishana uzoefu na kuweka mipango ya maandalizi ya mkutano wa COP 30 unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, 2025 nchini Brazil.

Ajenda ya Tanzania katika mkutano huo ni kuongeza upatikanaji wa fedha katika utekelezaji wa programu za mabadiliko ya tabianchi, nishati safi ya kupikia na kuhakikisha kuwa fedha zilizokuwa zimeahidiwa na wafadhili mbalimbali kwa  ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo zinatolewa kwa wakati.

Ajenda nyingine ni kushawishi wadau wa mazingira kutoa misaada yenye masharti nafuu ya kutekeleza programu za mazingira na kuwekeza katika teknolojia ya upimaji wa hewa ya kaboni ikiwa ni pamoja na kujengea uwezo taasisi zinazoratibu masuala ya mazingira nchini.

SOMA: Dira 2050 yataka uwezo kulinda mazingira

Kwa upande mwingine, Tanzania imeeleza nia yake ya kuendelea kutekeleza miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa njia ya ubia na kwa kutumia rasilimali zake za asili kama vile bahari, misitu, madini adimu, maziwa, mito pamoja na ujenzi wa  miundombinu rafiki kwa mazingira.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. After I originally commented I seem to have clicked the -Notify me when new comments are added-
    checkbox and now each time a comment is added I recieve four emails
    with the same comment. Is there a means you are able to
    remove me from that service? Kudos!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button