Tanzania yazindua ubalozi wa kudumu Austria
TANZANIA imezindua rasmi Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini Vienna nchini Austria.
Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Stergomena Tax amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo ni mafanikio yanayoimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Austria na Taasisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Vienna.
Amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo ni mafanikio makubwa ambayo yanaimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Austria na Taasisi za Umoja wa Mataifa zilizopo hapa jijini Vienna na inaonesha kwa vitendo kuwa Tanzania inaipa kipaumbele uhusiano wake na Austria.
Aidha, ameishukuru serikali ya Austria na Wizara inayoshughulikia masuala ya Ulaya na uhusiano wa Kimataifa kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi wa Tanzania Vienna tangu ulipoanzishwa hadi kufikia siku ya uzinduzi.
Nae, Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Ulaya na uhusiano wa kimataifa Peter Launsky-Tieffenthal amesema Austria inapongeza uamuzi wa serikali ya Tanzania wa kufungua Ubalozi wake Austria na kuungana na nchi nyingine 16 za Afrika zenye Ubalozi nchini humo na kuahidi kuusaidia Ubalozi huo kwa kila hali ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwake