TBS kushirikiana na kampuni 2 ubora wa magari

KATIKA kuhakikisha magari yanayoingizwa nchini, yanakuwa na ubora Shirika la Viwango Tanzania  (TBS),  limesaini mkataba na kampuni mbili zitakazosaidia kwenye mchakato wa kuwa na huduma bora za magari.

Akizungumza leo Juni 26, 2023 Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TBS,  Dk Yusuph Ngenya amesema wameingia makubaliano na kampuni za EAA na QISJ, ili kusaidia na kuwa na magari yenye ubora nchini.

“TBS hatuwezi kufanya kazi kila sehemu duniani, ndio maana  tumeona tushirikiane na wenzetu hawa kuhakikisha tunakuwa na ubora wa magari yanayoingizwa hapa nchini,” amesema.

Mwakilishi kutoka Kampuni ya QISJ, Brian Kuria amesema watashirikiana na TBS kuhakikisha magari yanayoingizwa Tanzania yanakidhi viwango.

“Lengo letu ni kuwasaidia Watanzania kupata magari bora,  tunatamani wafurahie huduma zetu na kujivunia ubora wa magari yatakayoingizwa,” amesema.

Takwimu zinaonesha kuwa zaidi ya magari 46,000 yanaingia nchini kwa mwaka, huku Japan ikiongoza kuingiza magari  ambapo asilimia 92 ya magari yanatoka nchini humo, huku asilimia  4 yakitoka nchini Uingereza.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button