SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limewataka wadu wa mpira wa miguu nchini kuacha kushirikiana na watu waliofungiwa kujihusisha na soka kwa sababu mbalimbali
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 20, 2023 kupitia taarifa rasmi ya Shirikisho hilo. “TFF inaendelea kufuatilia ukiukaji huo ili kuchukua hatua stahiki.”
Aidha, taarifa hiyo imeongeza kuwa wanafamilia wote wana wajibu wa kuzingatia katiba, kanuni na taratibu zinazoongoza mpira wa miguu.