KOCHA wa zamani wa Chelsea, Thomas Tuchel amekubali kuwa kocha wa timu ya taifa ya England.
Kwa mujibu wa BBC, Tuchel atakuwa meneja wa tatu wa Uingereza ambaye sio raia wa Uingereza kufundisha ya wanaume ya Uingereza baada ya Sven-Goran Eriksson na Fabio Capello.
SOMA: Ndoa ya Bayern, Tuchel kuvunjika Juni
Uingereza imekuwa bila meneja wa kudumu tangu Gareth Southgate alipojiuzulu kufuatia kushindwa kwa fainali ya Euro 2024 dhidi ya Hispania.
Lee Carsley, ambaye Chama cha Soka kilimteua kwa muda, atasalia katika nafasi yake kwa mechi mbili za mwisho dhidi ya Ugiriki na Jamhuri ya Ireland, huku Tuchel akitarajiwa kuchukua rasmi baada ya mechi hizo.
Utambulisho rasmi wa Tuchel unatarajiwa kufanyika Jumatano huko Wembley.
SOMA: Tuchel kuinoa Bayern
Comments are closed.