TISEZA kuanzisha madawati ya uwekezaji kwenye halmashauri

KAGERA: Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imewahaidi wawekezaji wazawa kuwa itaanzisha madawati ya uwekezaji kila halmashauri ili kuunganisha taasis ipamoja zinazohusiana na usajili wa maswala ya uwekezaji.

Taasisi ya TISEZA inaendelea na kampeni maalumu ya kuhamasisha uwekezaji kwa lengo la kusogeza huduma za uwekezaji hadi ngazi ya mikoa na halmshauri kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa taifa.
Akizungumza katika kongamano la wadau wa uwekezaji wa ndani mkoani Kagera, Mwenyekiti wa Bodi ya TISEZA, Balozi Azizi Mlima, amesema taasisi hiyo imelenga kutoa elimu ya uwekezaji kwa wananchi ili kuwawezesha kupata unafuu wa mitaji, pamoja na kusimamia utekelezaji wa sheria na taratibu za uwekezaji ikiwemo kuwapunguzia adha wawekezaji kwa kuweka dawati moja la kupata huduma zote.

Ameeleza kuwa licha ya changamoto ya uelewa mdogo wa uwekezaji kwa baadhi ya Watanzania, elimu na mipango ya TISEZA imeanza kuzaa matunda kwa kuwahamasisha wananchi kuwekeza zaidi ndani ya nchi, kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje na kukuza uzalishaji wa ndani.
Alisema TISEZA inaangazia fursa mbalimbali Kanda ya ziwa ikiwemo mkoa wa Kagera ambapo Kuna fursa nyingi za uwekezaji ikiwemo,Kilimo cha mazao ya biashara kama maparachichi
Ufugaji wa kisasa,Ufugaji wa samaki
Uongezaji thamani wa mazao ya kilimo ambapo Wananchi wamekumbushwa umuhimu wa kumiliki hati za nyumba na viwanja, kama nyenzo muhimu ya kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha na kuanzisha au kupanua miradi ya uwekezaji.

Wawekezaji ambao wameshiriki kongamano Hilo wamepongeza hatua muhimu za TISEZA Kuona umuhimu wa kufikisha elimuna kuweka mpango wa kufungua Madawati ya uwekezaji kwa ngazi ya halmashauri kama hatua muhimu ya kutambua changamotoo zao katika uwekezaji na kurahisisha hatua za kujisajili katika uwekezaji.



