TMDA yakamata dawa, vifaa tiba bandia

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imefanya oparesheni maalum ya siku nne ya ukaguzi na msako wa bidhaa za afya na kukamata dawa na vifaa tiba bandia na duni, dawa na vifaa tiba vya serikali na bidhaa zilizoisha muda wake.

Oparesheni hiyo imefanyika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Kigoma, Katavi, Mwanza, Simiyu, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Songwe, Lindi na Ruvuma huku maeneo yaliyokaguliwa yakiwa ni hospitali,zahanati,maghala,maduka ya dawa na maeneo mengine.

Advertisement

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo amesema oparesheni hiyo ilianza Novemba 20 hadi 24,2023 ambapo wilaya na mikoa husika ilichaguliwa kutokana na rekodi za matokeo ya miaka ya nyuma ya kaguzi za TMDA na taarifa za kiintelijensia.

Fimbo amesema katika oparesheni hiyo maeneo yaliyokaguliwa ni 777 kati yake 283 ni famasi,23 ni maduka ya vifaa tiba,tisa ni ghala za madawa,maghala ya vifaa tiba mawili, maduka ya dawa za mifugo 105,maduka ya dawa muhimu za binadamu 272,vituo vya kutolea huduma za afya 30,maabara 32 na kiwanda kimoja.

“Dawa za serikali zilikamatwa katika vituo binafsi vya kutolea huduma za afya ambazo ni pamoja na mseto ya kutibu malaria ya vidonge vya ALU,dawa ya kutibu kifua kikuu,dawa ya uzazi wa mpango na vifaa tiba na vitendanishi vya serikali vilikadhiriwa kuwa na thamani ya Sh milioni 11.3 vilikamatwa katika vituo na maduka binafsi,”ameeleza.

Amebainisha kuwa dawa zilizoisha muda wake zenye thamani ya Sh milioni 9.5 zilikamatwa zikiwa hazijatengwa kwa utaratibu unaotakiwa na vifaa tiba na vitendanishi vyenye thamani ya Sh milioni 10.3 vilikamatwa vikiwa havijatengwa.

Aidha amesema dawa bandia zilizokamatwa zilikuwa na thamani ya Sh milioni 5.8 ambapo dawa zote zilikuwa za mifugo na dawa duni zilizokamatwa zinathamani ya Sh 579,600 ambapo sehemu kubwa ya dawa hizo ilibainiska kusababishwa ba dawa husika kutotunzwa kwa kuzingatia maelekezo.

“Vifaa tiba na vitendanishi duni vya thamani ya Sh milioni 5.4 zilikamatwa na kuna bidhaa mabazo hazijasajiliwa dawa zenye thamani ya Sh milioni 133.3 zilikamatwa na vifaa tiba na vitendanishi ambavyo havijasajiliwa au kutambuliwa vyenye thamani ya Sh milioni 17.7.

Fimbo amesema oparesheni hiyo pia ilibainisha uwepo wa dawa zenye madhara ya kulevya kwenye maeneo mbalimbali zikiuzwa kwa siri.

Alifafanua kuwa katika majengo 777 yalifanyiwa ukaguzi majengo 200 yakutwa na bidhaa zisizosajiliwa,majengo 125 bidhaa zilizokwisha muda wake,majengo 84 hayakuwa na vibali,majengo 67 hayakuwa na mtaalamu.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *