TRA yasisitiza usajili wa biashara Geita

TRA yasisitiza usajili wa biashara Geita

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA), mkoani Geita imewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanasajili biashara zao, ili waweze kuziendesha katika mfumo rasmi na kwa mjibu wa sheria.

Hayo yameelezwa na Ofisa Elimu wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA Geita, Justine Katiti alipokutana na wafanyabiashara wa Kata ya Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita.

Katiti amesema ni vyema wafanyabiashara kuacha kuendesha biashara kienyeji, badala yake wahakikishe wanasajiliwa na kupata Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

Advertisement

Ameeleza kupata TIN ni utekelezaji wa sheria ya kodi na inatoa fursa za kuongeza mitaji ya biashara kutoka taasisi za fedha na kuingia katika ushindani wa masoko kimataifa.

Ameeleza Mkoa wa Geita una kampuni kubwa za uchimbaji wa madini zinazotoa tenda kwa wafanyabiashara waliosajili biashara zao na wanalipa kodi kwa mujibu wa sheria.

Aidha Katiti amesisitiza wafanyabiashara kuzingatia umuhimu wa kutunza kumbukumbu za biashara na utoaji wa risiti kwa kutumia Mashine za Kielektroniki (EFD).

Amesema risiti za EFD kwa wafanyabiashara wanaokidhi vigezo inasaidia kuondoa mkanganyiko wa ukadiriaji kodi na kuwezesha kila mmoja kulipa kodi halisi ya biashara zake.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *