MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Sh trilioni 2.47 Novemba mwaka huu ikiwa ni zaidi ya lengo la makusanyo kwa mwezi huo. Ofisa Mkuu wa Usimamizi wa Kodi TRA, Hamadi Mteri alisema hayo Dar es Salaam jana katika mku[1]tano na wafanyabiashara wa vifaa vya umeme Kariakoo.
Mteri alisema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wanaotoa wafanyabiashara pamoja na bidii wanayofanya katika kazi zao. “Tumepewa malengo, mwezi ulio[1]pita wa Novemba tulikuwa na lengo la kukusanya trilioni 2.4 kwa ush[1]irikiano wenu mliotusaidia tumevuka lile lengo, tumekusanya Sh trilioni 2.47 kwa hiyo tumekusanya zaidi ya lengo tulilowekewa,” alisema.
Mteri alisema kwa Desemba wanalenga kukusanya Sh trilioni 3.46 na kuwa malengo hayo ni makubwa kwa kuwa Desemba ni kati ya miezi inayoangukia kwenye ulipaji wa kodi ya mapato ambayo hulipwa Machi, Juni, Septemba na Desemba. “Mwezi huu tuna mzigo mzito zaidi sisi kama TRA kuliko mwezi uliopita, tunatakiwa tukusanye trilioni 3.4 wakati mwezi Novemba ilikuwa ni trilioni 2.4, ina maana kuna tofauti ya trilioni nzima na zaidi ukilinganisha na mwezi uliopita,” alieleza.
Mteri aliwaomba wafanyabiashara waendelee kuwaunga mkono kwa kuwawezesha kufikia malengo ya mwezi huu kama ilivyokuwa kwa mwezi Novemba. Vilevile, aliwakumbusha wafan[1]yabiashara hao mambo sita wanayo[1]paswa kuzingatia ili wasikumbane na changamoto katika uendeshaji wa biashara zao, Aliyataja ni urasimishwaji kwa kujisajili na kupata namba ya ut[1]ambulisho wa mlipakodi (TIN) na kuhakikisha wanafanyiwa makadirio ambayo yatamsaidia kwa aina yake ya biashara na kipato chake atapaswa kulipa kiasi gani.
Mengine ni pamoja na kutoa risiti ya mkono kwa wale ambao mauzo yao yapo chini ya Sh milioni 11 kwa mwaka, kwa mashine kwa wale ambao mauzo yao yanaanzia Sh milioni 11 na zaidi kwa mwaka na kuwasilisha ritani pamoja na kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka riba ya ucheleweshwaji