TRC yatapa hasara Sh bilioni 224

DAR ES SALAAM: MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amesema katika ripoti yake kuwa Shirika la Reli ( TRC) lilipata hasara ya Sh bilioni 224 katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikilinganishwa na Sh bilioni 102 mwaka uliopita.

Mkaguzi huyo amesema hasara hiyo ilichangiwa na kupungua kwa mapato ya usafirishaji kutokana na uhaba wa vichwa vya treni, mabehewa pamoja na mvua iliyosababisha kufungwa kwa njia kwa miezi minne.

Amesema shirika hilo lilitumia Sh bilioni 29.01 ruzuku kutoka serikalini. Ameongeza kuwa kama ruzuku hiyo isingetolewa shirika lingepata hasara ya Sh bilioni 253.

CAG Kichere ameeleza kuwa taarifa hiyo inahusu kipindi kilichoishia Juni 30, 2024 kabla ya kuanza kutumika kwa reli ya SGR.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button