Trump aondoa vikwazo kwa Syria

WASHINGTON DC : SERIKALI ya Marekani imeiondolea Syria baadhi ya vikwazo, kufuatia kutiwa saini kwa mkataba wa makubaliano kati ya nchi hizo mbili, hatua iliyolenga kuimarisha amani na utulivu nchini humo.

Hatua hiyo imekuja takribani mwezi mmoja na nusu baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza nia ya kuondoa vikwazo hivyo wakati wa ziara yake Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Karoline Leavitt, makubaliano hayo yanalenga kuunga mkono juhudi za serikali mpya ya Syria katika kurejesha utulivu, mshikamano wa kitaifa, na ushirikiano wa kimataifa.

SOMA:Marekani Ufaransa kuijadili mashariki ya kati

Leavitt amesema pamoja na hatua hiyo ya kuondoa baadhi ya vikwazo, bado vikwazo dhidi ya aliyekuwa Rais wa Syria, Bashar al-Assad, na washirika wake, vitaendelea kubaki palepale.

Tangu kuondolewa madarakani kwa Assad mnamo Desemba mwaka jana, serikali mpya ya Syria imekuwa ikifanya jitihada za kurejesha uhusiano na jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na kutaka vikwazo vyote kuondolewa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button