WASHINGTON DC : RAIS wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa anatarajia kutoa uamuzi kuhusu Iran kwa muda mfupi ujao, baada ya mazungumzo yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili yaliyofanyika nchini Oman.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika Air Force One, Trump alieleza kuwa amekuwa na mkutano na washauri wake kuhusu hali hiyo, ingawa hakuweka wazi maelezo zaidi.
Kauli yake inakuja huku Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, akiwa hajasema lolote rasmi kuhusu mazungumzo hayo, licha ya kushiriki katika mkutano ambapo alisisitiza umuhimu wa kuanza kujiandaa.
Hatahivyo Trump amesema matumaini makubwa yapo kuhusu mazungumzo hayo “sidhani kama kuna haja ya kusema mengi mpaka yatakapokamilika, lakini mambo yanaonekana kuwa mazuri”, alisema Donald Trump.