MAREKANI : WAZIRIMKUU wa Israel Benjamin Netanyahu anakutana leo na Rais wa Marekani Donald Trump.
Netanyahu atakuwa kiongozi wa kwanza kutembelea Ikulu ya White House tangu Trump aliporejea madarakani mwezi uliopita.
Katika kikao hichi , viongozi hawa wawili watajadili kuhusu mustakabali wa makubaliano ya pamoja ya kuvimaliza vita katika Ukanda wa Gaza. SOMA: Netanyahu kukutana na Trump wiki ijayo
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Netanyahu imesema kuwa Israel itapeleka ujumbe mjini Doha, Qatar baadae wiki hii kwa ajili ya mazungumzo mapya.
Kundi la Hamas limesema liko tayari kujadili hatua ya pili ya usitishaji huo wa mapigano unaosimamiwa na Qatar, Misri na Marekani.