Netanyahu kukutana na Trump wiki ijayo

MAREKANI : WAZIRIMKUU wa Israel Benjamin Netanyahu atakutana na Rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House wiki ijayo.

Ofisi ya Netanyahu ilisema ziara hiyo itafanyika tarehe 4 Februari na kwamba alikuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kualikwa katika Ikulu ya White House wakati wa muhula wa pili wa Trump.

Afisa wa Ikulu ya White House alithibitisha kwamba kutakuwa na mkutano mapema wiki ijayo, lakini akasema tarehe na wakati bado havijahitimishwa.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, Rais Donald Trump alisema Netanyahu atasafiri kwenda Washington kukutana naye “hivi karibuni sana”, lakini hakutoa tarehe maalum.

SOMA: Hamas yakubali rasimu ya kusitisha mapigano Gaza

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button