Tughe, taasisi zapongeza ongezeko likizo ya uzazi

DAR ES SALAAM: Chama wa Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE) kwa kushirikiana na Taasisi za Doris Mollel Foundation wameishukuru Serikali kupitia Bunge la Tanzania kupitisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Kazi (NA.13) wa Mwaka 2024 ambapo umeongeza likizo ya uzazi kwa wanaojifungua watoto njiti kufikia wiki 40 kwa mama anayejifungua na siku saba kwa baba wa mtoto huyo.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa TUGHE Dk.Jane Madete amesema hatua hiyo ni ya kupongeza kwa sababu wamekuwa wakilipigania kwa muda mrefu lakini pia ni hatua muhimu ambayo itasaidia kulinda ustawi wa watumishi.
Amesema Taasisi ya Doris Mollel inatambua umuhimu wa kuongeza siku za likizo kwa wazazi wanaopata Watoto njiti kwani kutalinda ustawi wa afya za Watoto wanaozaliwa kabala ya wakati ambao wanahitaji mud awa kutosha wa Uangalizi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Foundation Doris Mollel amesema Hatua hiyo ni kubwa kwani huu si ushindi wa akina na mama tu, bali ni ushindi wa Tanzania kuwa kuwa Tanzania imeandika historia na itakuwa ni mfano wa kuigwa kwa mataifa yote .
Itakumbukwa kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa maombi yaliyotolewa na Chama cha wafanyakazi katika sherehe za wafanyakazi zilizofanyika Mei Mosi 2024 mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango kwa niaba ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.



