Tume kutumia wiki mbili kuamua rufaa za watumishi
DODOMA: TUME ya Utumishi wa Umma inatarajia kutumia takribani wiki mbili kwa ajili ya kujadili na kutoa uamuzi wa rufaa na malalamiko yaliyowasilishwa na watumishi wa umma kwa tume hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dodoma, Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, John Mbisso alisema kazi hiyo itafanyika katika mkutano wa tatu wa Tume kwa mwaka 2025/26 ambao umepangwa kuanza Machi 23 hadi Aprili 15 mwaka huu.
“Mkutano huo utafanyika jijini Dodoma kuanzia Machi 23 hadi Aprili 15 mwaka huu kwa siku za kazi na utakuwa na jukumu la kujadili na kutoa uamuzi wa rufaa na malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa na watumishi wa umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na waajiri, mamlaka za ajira na mamlaka zao za nidhamu katika utumishi wa umma.”
Kwa mujibu wa kifungu cha 12(1)(d) na kifungu cha 27(1)(b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Tume ina jukumu la kupokea na kushughulikia rufaa na malalamiko ya watumishi wa umma ambao hawajaridhika na uamuzi uliotolewa na waajiri, mamlaka za ajira na mamlaka za nidhamu katika utumishi wa umma.
Aidha, Mbisso alisema katika mkutano huo, Tume itatoa nafasi kwa warufani na warufaniwa walioomba kufika mbele ya Tume kutoa ufafanuzi wa ziada kuhusu hoja zao za rufaa.
“Kanuni za Utumishi wa Umma zimeipa uwezo Tume wa kutoa nafasi kwa rufani au warufaniwa kufika kwenye tume kutoa maelezo ya ziada kama tu wameomba tume imsikilize. Kwa hiyo walioomba watapewa fursa ya kutoa maelezo ya ziada ili kuifanya Tume kuwa katika nafasi nzuri ya kutoa uamuzi wa haki kwa pande zote husika.”
“Pindi wanapofika mbele ya Tume awe warufani na warufaniwa anaruhusiwa kuja na mtu ambaye anaona anaweza kumsaidia katika suala lake lililombele ya Tume, anaweza kuwa mwanasheria, au mtumishi wa umma au chama cha wafanyakazi.”
Mbisso alisema katika mkutano huo, pia tume itapitia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa majukumu ya tume zitawasilishwa, kujadiliwa na kutolewa maelekezo kwenye mkutano huo.



JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com