Tume ya Chande yafika mikoa 11 kuchunguza ghasia

DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Oktoba 29, Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande, amesema awali tume ilipanga kutembelea mikoa sita iliyoathiriwa zaidi na ghasia, lakini baadaye iliongeza wigo na kufikia mikoa 11 pamoja na wilaya 22 ili kujifunza kwa upana maeneo yaliyoathiriwa na yasiyoathiriwa.

Amesema katika zoezi la kusikiliza wananchi, tume ilifika Kilimanjaro na Zanzibar ambako hakukuwa na madhara ya ghasia za Oktoba 29, ikilenga kujifunza uzoefu wa maeneo yaliyobaki salama.

Alieleza kuwa Zanzibar ilichaguliwa makusudi kutokana na uzoefu wake wa maridhiano, akisisitiza kuwa Tume inalenga kupendekeza suluhu za maridhiano baada ya kukamilisha kazi yake.

Aidha, alitaja Mkoa wa Kilimanjaro kuwa mfano wa eneo ambalo halikukumbwa na vurugu licha ya kuwa jirani na maeneo yaliyokumbwa na matukio hayo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button