Tume yakutana na wananchi Dodoma

TUME ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Februari 5, 2026, imekutana na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma waliofika kutoa ushahidi wao.

Mkutano huo wa Tume na wananchi hao umefanyika katika Ukumbi uliopo ghorofa ya pili katika Jengo la Takwimu lililopo mkoani Dodoma. Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.

Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo ambapo kwa Dodoma tume inaendesha shughuli zake katika Ukumbi wa Takwimu, kwa Mkoa wa Iringa Tume ipo Ukumbi wa Siasa ni Kilimo na kwa Shinyanga Tume ipo katika Ukumbi wa Manisapaa ya Kahama. SOMA: Tume yatua Dodoma yakutana na RC, Kamati ya Ulinzi

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button