‘Tuongeze uzalishaji wa nguzo za zege’

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imetembelea na kukagua mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa nguzo za zege (TCPM) kilichopo mkoani Tabora kwa lengo la kujiridhisha na utekelezaji wake. Kamati hiyo imeishauri Serikali kuongeza idadi ya viwanda vya uzalishaji wa nguzo hizo ili kusaidia kukidhi mahitaji ya miundombinu ya umeme nchini.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Subira Mgalu amesema mahitaji ya nguzo za umeme kwa sasa nchini ni takribani nguzo laki mbili, huku uzalishaji wa sasa ukiwa takribani nguzo elfu themanini pekee. Amesema licha ya kamati kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika uzalishaji huo bado kuna umuhimu wa kuongeza uzalishaji zaidi kwa kushirikisha wawekezaji wa sekta binafsi ili kukidhi mahitaji yaliyopo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati Dk. Deogratius Ndejembi, amesema Serikali tayari imeweka mpango mkakati wa kujenga viwanda zaidi vya uzalishaji wa nguzo za zege, ikiwemo katika mkoa wa Mbeya, ili kuongeza uzalishaji nchini. SOMA: Serikali kuweka vituo kupoza umeme kila wilaya

Aidha, kamati hiyo pia imetembelea kiwanda cha uzalishaji wa mkaa mbadala cha Rafiki Briquettes na kukitaka kuanza uzalishaji mara moja, huku Serikali kupitia STAMICO ikiwa tayari imetoa zaidi ya shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kukamilisha mradi huo utakaosaidia kuongeza ajira na kuchangia maendeleo ya uchumi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button