‘Tuzo za watendaji, wakuu wa kampuni 100 bora kuchochea ufanisi’

DAR ES SALAAM: TUZO za wakuu na watendaji wa makampuni 100 bora hapa nchini zimetajwa kuwa ni njia sahihi ya kutoa chachu maendeleo kwa kuwa itahamasisha ufanisi kazini.

Ukiwa ni msimu wa tatu wa tuzo hizo hapa nchini, ‘Tanzania Top 100 Executive Awards” tukio hilo huandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwatambua watendaji wakuu wa makampuni mbalimbali wanaofanya vizuri hapa nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Eastern Star, Deogratius John Kilawe ametamka hayo jijini Dar es Salaam,  Novemba 24, 2023, katika tukio la utoaji wa tuzo hizo ambalo liliwaleta pamoja watendaji na wakuu wa makampuni mbalimbali nchini.

Pamoja na mambo mengine, tuzo hizo zimelenga kutambua na kuthamini kile kinachofanywa na watendaji wa kampuni Tanzania ikiwa ni moja kati ya jitihada na harakati za kuchochea ukuaji na kuwatia moyo wa kuendelea kufanya vizuri zaidi na kuleta chachu ya maendeleo.

Miongoni mwa sifa kuu za kushiriki shindano hilo, kwa mujibu wa Kilawe, ni pamoja na kampuni au mfanyabiashara kuwa na pato linaloanzia Shilingi Bilioni 1 na kuendelea na kuwa na hati safi za ukaguzi wa mahesabu ya kampuni kwa miaka mitatu iliyopita.

Ameongeza ya kwamba, kwa miaka 3 Sasa Eastern Star Grup imekuwa ikiratibu kwa mafanikio tuzo hizo nchini Tanzania ambako wamekuwa wakifanya uchunguzi wa huduma mbalimbali za kibiashara na kuchangia ustawi, maendeleo na mafanikio ya kampuni shiriki na taifa kwa ujumla.

“Tumefanya utafiti yakinifu na wa kina ili kuwapata wakuu na watendaji wa kampuni 100 bora nchini. Tunaamini kupitia mchakato huu utasaidia kutoa fursa kwa washiriki hao na kunufaika zaidi,” amesema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button