IMEELEZWA ‘Twitter’ imepoteza karibu nusu ya mapato yake ya matangazo tangu iliponunuliwa na Elon Musk kwa Dola bilioni 44 (£33.
6bn) Oktoba mwaka jana.
Alisema kampuni hiyo haijaona ongezeko la mauzo ambalo lilitarajiwa mwezi Juni.
Huenda hatua hiyo imechangiwa na Musk kuwafuta kazi takribani nusu ya wafanyakazi 7,500 wa Twitter alipochukua wadhifa huo mwaka wa 2022 katika juhudi za kupunguza gharama.
Mpinzani wa mtandao huo, Threads sasa una watumiaji milioni 150, kulingana na makadirio yaliyopo.
Wakati huo huo, Twitter inajitahidi kupambana na mzigo mkubwa wa madeni huku mtiririko wa pesa ukiwa mbaya.
Musk alisema mwishoni mwa wiki, ingawa hakuweka wazi muda wa kushuka kwa 50% ya mapato ya matangazo.
Katika tweet alisema: “Tunahitaji kufikia mzunguko mzuri wa pesa kabla ya kuwa na anasa ya kitu kingine chochote.”
Baada ya kuachisha kazi maelfu ya wafanyikazi na kupunguza bili, Musk alisema Twitter ilikuwa njiani kuchapisha mapato ya $3bn (£2.29bn) mnamo 2023, kutoka $5.1bn mnamo 2021.