‘Uamuzi kuhamisha wananchi ulikuwa sahihi’

TUME ya Rais ya Kutathmini Uhamaji wa Hiari ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro imesema uamuzi wa serikali wa kuhamisha wananchi kwa hiari ulikuwa sahihi, ingawa utekelezaji wake haukufikia matarajio kutokana na changamoto za uratibu, ushirikishwaji wa wananchi na mabadiliko ya miongozo.
Mwenyekiti wa tume hiyo, Katibu Mkuu mstaafu Musa Iyombe, amesema wakati tume ikikagua kaya 1,678 sawa na asilimia 7.3 ya kaya 23,000 na mifugo 40,593 sawa na asilimia 5.7 ya mifugo 715,466, ilibainika kuwa uhamaji wa hiari ni jambo la msingi na unahitaji kuratibiwa, kusimamiwa na kutekelezwa ipasavyo.

Iyombe amesema serikali tayari imewekeza Sh. bilioni 212.35 kuhamisha wananchi pamoja na nyumba 1,559 zilizojengwa Msomera ambazo hazijapatiwa wakazi, huku huduma za kijamii zikifanywa kwenye maeneo yaliyotengwa ili kufanana na Hifadhi ya Ngorongoro. SOMA: Kaya 77 zenye watu 463 zaagwa Ngorongoro.
Tume imependekeza marekebisho ya sheria na kanuni za hifadhi ili kuondoa dhana za kibaguzi, kuimarisha usimamizi wa watu, mifugo na ujenzi wa majengo. Pia inapendekeza serikali kuwapa wananchi fedha badala ya kujengewa nyumba, jambo linalopunguza gharama na kuheshimu mila na tamaduni za jamii.
Aidha, tume inapendekeza kuundwa kwa chombo huru cha kuratibu uhamaji wa hiari, pamoja na mpango wa ushirikishwaji wa wananchi na wadau muhimu, ikiwemo elimu kwa wananchi, madiwani, viongozi wa kimila na dini. Mapitio ya mwongozo wa utekelezaji na utumiaji wa motisha pia yamependekezwa ili kuepusha malalamiko na kuhakikisha zoezi linafanyika kwa ufanisi.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com