Uanzishwaji wa bima kunufaisha wananchi Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema uanzishwaji wa huduma mpya ya Bima ya Takaful ni hatua muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za bima kwa wananchi ili kuchochea maendeleo ya Shirika la bima Zanzibar(ZIC).

Dk Mwinyi ameyasema hayo leo alipozindua kampuni tanzu ya ZIC TAKAFUL ambayo ni kampuni inayotoa huduma za bima kwa kufuata misingi na sheria za dini ya Kiislamu iliyoanzishwa na Shirika la bima la Zanzibar (ZIC).

Amesema kupitia wataalamu wa Bima Takaful ni kiungo muhimu katika ukuaji wa huduma za fedha zinazofuata misingi ya Kiislamu kwa sababu huduma hiyo hutoa fursa kwa mabenki ambayo tayari yanaendeshwa kwa misingi hiyo , kuweza kutoa huduma za bima jambo halikuwezekana kabla ya uanzishwaji wa Takaful.

Advertisement

AidhaDk Mwinyi amewakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa kuja kuwekeza katika huduma za bima za aina hii ya Takaful ili waweze kuongeza uwezo wa kukatia bima miradi mikubwa itakayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *