Ubakaji wanafunzi Simiyu hali sio salama
VITENDO vya ukatili wa kijinsia hususani matukio ya ubakaji, ulawiti na matendo mengine kama hayo vimeendelea kuwa mwiba kwa baadhi ya wanafunzi wa kike ukiachia mbali changamoto zingine zinazowakabili hasa wanaosoma katika madaraja ya chini ya elimu ikiwemo Shule za Msingi na Sekondari Mkoani humo.
Miongoni mwa changamoto hizo ni kushamiri kwa vitendo vya ubakaji na ulawiti na matukio mengine kama hayo ambapo vitendo hivyo hufanyiwa watoto walio chini ya miaka 18 hasa waishio vijijini na mara kadhaa maeneo ya mijini.
Moja kati ya hayo matukio ni liliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na kufunguliwa jarada la upelelezi namba BAR/RB/654/2024, ni tukio lililotokea kwa mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Mahaha, (jina limehifadhiwa) ambaye alipatwa na mkasa wa kubakwa na mwanaume aliyefahamika kwa Jina la Elisha Mboje Mei 28, 2023 Alhamisi alipokwenda kuchuma nyanya alizokuwa ameagizwa na bibi yake katika shamba lililopo jirani na eneo la Mto Mahaha.
Mto huo unatenganisha kata ya Sima na Mahaha katika Halmshauri ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, ambapo hadi hivi sasa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ikiwemo kumkamata Mtuhumiwa aliyetambulika kwa Jina la Elisha Mboje aliyefanya tukio hilo Alhamisi Machi 28, 2024 na kisha kutoweka mara baada ya upelelezi wa kesi hiyo kuanza na hatua za kumkamata zikichukuliwa.
Katika mahojiano maalumu na HabariLeo aliyofanya mwishoni mwa wiki hii, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mahaha iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, Revocatus Manyenya amezitaka taasisi husika zinazoshughulikia masuala hayo ya kupinga vitendo vya ukatiri dhidi ya watoto wa kike kuchukua hatua ikiwemo kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa wa kesi hiyo ya ubakaji inayomkabili kwa kuwa tayari mhusika anafahamika.
Ameeleza kuwa kutokana na kutochukuliwa uzito wa suala hilo hasa kwa ngazi ya polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kumchukulia hatua mshitakiwa aliyetambulika kwa jina la Elisha Mboje imepelekea mtuhumiwa huyo kufanikiwa kutoroka na kusababisha ushahidi uliopatikana dhidi yake katika hatua za awali kutokuwa na manufaa katika kesi hiyo ya jinai yenye RB No. BAR/RB/564/2024.
Anasema kuwa tukio kama hilo la ubakaji alilofanyiwa mwanafunzi huyo katika shule yake ni la pili kutokea shuleni hapo ambapo ameshatolea taarifa zake katika mamlaka husika lakini ufuatiliaji ili haki iweze kutendeka imeonekana kuwa ni changamoto kwa kwa hapo.
Hata hivyo katika uchunguzi wa awali uliofanya na gazeti hili, kwa muda mfupi katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi katika Shule ya Sekondari Bariadi iliyoko Kata ya Somanda kuliripotiwa tukio lingine la mwanafunzi mwingine wa kidatocha tatu ambaye naye alifanyiwa vitendo hivyo na alipohojiwa na uongozi wa shule alikiri kufanyiwa vitendo hivyo.
“Mbali na hili la huyu mwanafunzi wa kidato cha pili pia tunalo tukio lingine la mwanafunzi wa kidato cha nne mwenye RB No. 4942024 ambalo pia taarifa zake zilishafikishwa katika vyombo husika ikiwemo Jeshi la Polisi na hakuna hatua stahiki iliyochukuliwa hali inayotufanya tuwe na wasi wasi zaidi kwa kuwa idadi kubwa ya Wanafunzi shuleni hapa wanaishi mazingira yaliyo mbali na shuleni hivyo hutembea umbali mrefu tena maeneo hatarishi,” alieleza.
Uchunguzi wa HabariLeo pia ulifika hadi katika maeneo ambayo yamekuwa yakilielezwa kuwa ndipo matukio ya ubakaji hufanyika hususani kwa lililomtokea mwanafunzi huyo wa Mahaha Sekondari na kupata taarifa kwa viongozi wa kijiji hicho ambapo baadhi ya wakazi wa Meneo hayo lililoko katika kata ya Sima, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa wa Ngashanda, Masangu Hasara ameeleza kuwa matukio ya aina hiyo yamezidi kushamiri hususani kwa watoto wanaokaa mbali na maeneo ya shule ambao hulazimika muda mwingine kuvuka Mto Mahaha ili kufika shuleni hapo.
Bw. Hasara ameitaka Serikali ifungue barabara kutoka Ngashanda kwenda Bariadi mjini inayopitia eneo la Gitoya kwa kwa wanafunzi wamekuwa wakihangaika kupita katika Pori hilo mida ya asubuhi na jioni ambapo shule zao wameelekeza kuanza safari kuelekea Shuleni saa 11 alfajiri, na kurudi jioni ambapo giza linakua limeanza na kutokana na hali hiyo matukio mengi ya ubakaji yamekuwa yakifanyika mida hiyo ya Wanafunzi wakienda shuleni ama kurejea nyumbani.
“Ukiangalia kwa sasa pori ni kubwa na watoto wamekuwa wakiagizwa kuanza safari saa 11 alfajiri ili kuwahi Shuleni, hivyo tunaomba Serikali kama inasikia kilio chetu ifungue njia hii ya Ngashanda kuelekea Gitoya ambapo kuna mito zaidi ya miwili na pori kubwa ambapo pia Wanafunzi hutakiwa kulivuka ili kufika shuleni kwao hasa wanaotoka Ngashanda kuelekea Simiyu Sekondari na wanaotoka Gitoya kwenda Mahaha Sekondari,” amesema.
Pia kwa upande wa wazazi walizungumza na mtandao huu, wameitaka Seriali kufanya maboresho ya njia inayokatiza katika pori hilo wa kuwa msimu wa mvua unapoanza kunyesha vitendo hivyo hukithiri kwa kuwa vichaka huongezeka na kuwafanya wabakaji kujificha katika maeneo hayo kwa muda wote mchana na usiku.
“Tunaonda pori hili lifyekwe kwa tumechoka kubakwa, sasa unakuta sisi wazee tukitoka mashambani tnakutana na vikundi vya vijana wanaojificha hapa na kufanya matukio haya ya ubakaji, hali hii imekuwa hatarishi kwa maisha yetu wanawake na watoto wa kike wanaoenda mashuleni kwa kutumia njia hii,” anaeleza Kija Dwasi mkazi wa Ngashanda.
“Tunaomba pori hili lifyekwe kwa tumechoka kubakwa, sasa unakuta sisi wazee tukitoka mashambani tnakutana na vikundi vya vijana wanaojificha hapa na kufanya matukio haya ya ubakaji, hali hii imekuwa hatarishi kwa maisha yetu wanawake na watoto wa kike wanaoenda mashuleni kwa kutumia njia hii,” anaeleza Kija Dwasi mkazi wa Ngashanda.
Naye, Mwakilishi wa Shirika Lisilo la Kiserikali la Haki Elimu Tanzania katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ambaye pia ni Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Bariadi, Janeth Kato ameeleza kuwa wakati ndani ya familia vitendo hivyo vatajwa kufanywa na wanandugu, wanafunzi wengi hawana amani hasa wanapokwenda ama kurudi shuleni kwa kutumia njia ambazo ni hatarishi ikiwemo aliyokuwa akiitumia mwanafunzi huyo ambayo inamlazimu kuvuka mto Mahaha ili afike nyumbani kwao.
“Ukiangalia mazingira mengi ya eneo ambako Shule ipo kuna nyumba ziko upande wa pili wa mto huo hivyo ni lazima mwanafunzi avuke mto Mahaha ili aweze kufika shuleni kila siku, na hali ikiwa mbaya ya mvua huwabidi kupita daraja linalotenganisha Kata ya Sima na Mahaha ili waingie upande wa pili wanapoishi,” alisema.
Kwa upende wa baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi hao wameelezea hali ya kutokuwepo kwa usalama kwa Wanafunzi hao na kuitaka Serikali kuja na utatuzi wa changamoto hiyo akiwemo Anna Lushiba ameitaka Serikali kuchukua hatua ya kuliondoa pori hilo kwa kuwa wanawake wa maeneo hayo yamechoshwa na matukio ya ubakaji yanayoendelea katika pori hilo.
“Wanawake tumechoshwa na matukio haya ya ubakaji, tumekuwa tukivamiwa na Vijana wanaojificha katika Pori hili ambapo huwabaka Wanawake, sasa mtu mzee kama mimi nitafanya nini kwa hali kama hiyo, hivyo kero yetu sisi tunaiomba Serikali isafishe pori hili ili kuoondoa matukio yanayoweza kusabisha taharuki kwa jamii na muda mwingine kusababishwa vifo visivyo tarajiwa,” amesema.
Hata hivyo alipofikiwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu, Edith Shebe alikiri kupata taarifa za matukio mawili ya wanafunzi hao na alizitaka familia ya binti huyo wa Mahaha sekondari kufika kituoni kwake ili aweze kusikiliza shauri la kesi hiyo na kuanza kulifanyia kazi ili haki iweze kutendeka.
“Kutokana na uhitaji wa uchunguzi wa kina juu ya kesi hii huwa tunashauri familia nazo ziweze kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi ili haki iweze kutendeka kwa kuwa bila taarifa za kina za ufanyikaji wa tukio hilo, muda mwingine inakuwa ngumu kuweza kumbaini aliyefanya tukio hilo, hivyo tunashauri familia nayo ione uzito wa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili uchunguzi uanze ili kubaini aliyefanya tukio hilo ni nani,” alisema.
Alisema kuwa endapo taarifa za awali zikikusanywa kwa umakini hasa za kufanyika kwa tukio hilo, kunatoa urahisi kwa mhanga kupata haki yake na kusaidia jeshi la polisi kubaini aliyefanya tukio hilo, hivyo tunashauri wazazi au walezi wa binti huyo waje ofisini ili kusikilizwa kwa kesi yao ili haki iweze kutendeka.
Hata hivyo, HabariLeo ilifanya mawasiliano mara kadhaa na mlezi wa binti huyo ambaye ni bibi yake pamoja na uongozi wa kijiji kuweza kuileta kutuoni hapo ili waweze kupatiwa msaada kama familia hiyo ajili ya taratibu zingine hazikuzaa matunda kwa kuwa licha ya kuweza kuwezeshwa kifedha kwa ajili ya nauli waweze kufika katika Kituo cha Polisi hawakuonyesha kutoa ushirikiano wa kuweza kufika kituoni kwa muda ambapo RPC alishauri ili kesi yao iweze kusikilizwa.