Uchafuzi wa mazingira wasababisha saratani ya mapafu

ASIA : UCHAFUZI wa mazingira umebainika kuwa chanzo kikuu cha ongezeko la  aina ya saratani ya mapafu ambayo inaathiri watu wasiovuta sigara, ikiwa ni pamoja na wanawake na makundi mengine maalum.

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la Lancet Respiratory Medicine kwenye maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani, takriban watu milioni 2.5 waligundulika kuwa na saratani ya mapafu mwaka 2022.

Ongezeko hili linatokana na mabadiliko ya kimazingira, hasa uchafuzi wa hewa ambao unachochea kuenea kwa ugonjwa huo. SOMA: Saratani yaendelea kuwa tishio

Advertisement

Hata hivyo, ingawa utafiti umeonyesha kuwa wanaume ndio wengi zaidi wanaokumbwa na ugonjwa huu, wanawake nao wameonesha ongezeko la karibu milioni moja katika visa vya saratani ya mapafu.

Aina ya saratani ya mapafu inayosababisha athari kubwa kwa wanawake ni adenocarcinoma, ambayo inatajwa kuathiri zaidi wanawake katika zaidi ya nchi 185 duniani.

Utafiti huu pia umebainisha kuwa maeneo kama Kusini Mashariki mwa Asia yanakabiliwa zaidi na ongezeko la visa hivi, na kwamba uchafuzi wa hewa ni moja ya sababu kuu zinazochochea tatizo hili kubwa.

 

 

1 comments
  1. It is in reality a great and useful piece of
    info. I am satisfied that you just shared this helpful
    information with us. Please keep us informed like this.
    Thank you for sharing.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *