Ujenzi Makumbusho ya Mwalimu Nyerere Dodoma safi!

RAIS wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan , ameridhia kujenga Kituo Kikubwa cha Kumbukumbu ya hayati Mwalimu Julius Nyerere mkoani Dodoma ili kuenzi na kuhifadhi historia ya taifa.
Akizungumza katika mahojiano maalum na DailyNews Digital , Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere, Paul Kimiti amesema uamuzi huo ni wa busara hasa ukizingatia Dodoma ni mji mkuu wa serikali.
“ Namshukuru mheshimiwa Rais Samia , nilipoomba kuanzisha museum kubwa pale Dodoma ya Mwalimu Nyerere serikali ikakubali , kwa sababu viongozi mbalimbali kutoka nje wanakwenda Dodoma,” amesema Kimiti na kuongeza: “Butiama ni pazuri kuna vitu vyake vitaendelea kuheshimiwa lakini ukitaka vitu vya kumbukumbu vya Mwalimu Nyerere vitakaa pia Dodoma.“
Ameongezea kuwa hivi sasa wadau mbalimbali wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi wameshaanza kuulizia kuhusu ujenzi wa kituo hicho. “Watu wa nje wameshaanza kuuliza huu ujenzi unaanza lini,” alisema. SOMA: Dk Mpango: Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kufanya kazi
Katika historia ya Tanganyika hadi Tanzania ,Mwalimu Nyerere alitaka kuona shughuli zote za serikali zinafanyika katika Mkoa wa Dodoma, jambo ambalo tayari serikali imeshaanza kutekeleza . Amsema kuwepo kwa Kituo Maalumu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika mkoa wa Dodoma italiwezesha taifa kuenzi na kuhifadhi historia ya taifa katika harakati za kuikomboa Tanganyika hadi Tanzania.


