Ukimwi kutokomezwa Tanzania ifikapo mwaka 2030

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, amesema Tanzania imejipanga kuutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030.

Pia amesema hadi sasa asilimia  96 ya Watanzania wanaoishi na VVU wanajua kuwa wana maambukizi,  asilimia 98 ya wanaoishi na VVU wanatumia dawa za ARVs na asilimia 97 ya wanaotumia dawa wamefubaza makali ya UKIMWI, hivyo amesisitiza safari ya kutokomeza UKIMWI ifikapo mwaka 2030 itakamilika.

“Mafanikio haya yamechangiwa na utashi wa kisiasa ambapo Rais wetu Dk Samia Suluhu amekuwa mstari wa mbele kuongoza na kuwezesha upatikanaji wa rasilimali katika mapambano dhidi ya UKIMWI, ambapo uratibu wa masuala ya UKIMWI nchini upo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Tanzania pia imekuwa ikizingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na WHO/UNAIDS ili kutokomeza UKIMWI ikiwemo kuanzisha Sera ya Kupima na Kutoa Dawa (Test and Treat) kwa Watu wanaobainika kuwa VVU bila kusubiri kigezo cha idadi ya CD4, utoaji dawa za kuzuia maambukizi ya VVU kwa makundi yenye hatari zaidi ya kuambukizwa VVU.

“Kurahisisha utoaji wa ARVS kwa kuanza afua ya kutoa dawa za muda wa miezi mitatu hadi sita, utoaji wa Kondomu hadi kwenye ngazi ya jamii na kuongeza upimaji wa VVU kwa kuanzisha huduma ya kujipima VVU navyo vimechangia mafanikio haya,” amesema.

 

Habari Zifananazo

Back to top button