Wataalamu wapewa mafunzo kutibu uti wa mgongo

DAR ES SALAAM; Zaidi ya Wataalumu wa Afya 100 wa Ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Duniani wameanza kupatiwa mafunzo ya uti wa mgongo kwa siku tatu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 20 hadi 22,2026 Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Dk Lemeri Mchome amesema kuwa asilimia 60 ya wagonjwa waliopo katika taasisi hiyo wanasubuliwa na maumivu ya uti wa mgongo.

“Tatizo hili la maumivu ya uti wa mgongo ni kubwa sio Tanzania tu hata nchi zingine kwa hapa MOI asilimia 60 wanakuja na wnamaumivu hivyo ni sehemu inayohitaji uwekezaji mkubwa hasa wa kutoa mafunzo kwa wataalmu ya namna ya kutibu kisasa.

Amesema zaidi ya wataalamu 150 kutoka Marekani,Ulaya, Liberia, Uganda, Congo na nchi nyingine za Afrika watapata mafunzo kwa vitendo pia katika taasisi ya MOI ambayo ambapo serikali imewekeza kwa kununua vifaa vya kisasa zaidi.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Uti wa mgongo,Ubongo na Mishipa ya fahamu Hamisi Shabani amesema kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Well cornel kilichopo Newyork, Marekani wamejifunza vitu vingi na wamewasaidia kuboresha huduma nchini.

“Kozi ya mwaka huu ni ya 12 na inakwenda kujadili matatizo sugu ya uti ya mgongo ambayo watanzania waliowengi wanaumwa .Kozi hii inasehemu ya majadiliano, kujifunza ,kubadilisha ujuzi na kufanya mafunzo kwa vitendo na tunatarajia kutibu wagonjwa 20.

Naye Mkufunzi kutoka Weill Cornell Medicine Prof. Roger Hartly amesema kutokana na ukubwa wa tatizo inahitaji mafunzo zaidi ili kuimarisha wataalamu kutoa huduma kwani wanapenda kuwasaidia wananchi.

Amesema MOI ilikwenda Marekani na walijadili namna tunaweza kuwasaidia wananchi katika tatizo la uti wa mgongo na wameungana kufanya kitu

“Tanzania tatizo linakua na katika hili matibabu sio tu upasuaji pia mazoezi yanahusika.Tunapenda kushirikiana ili kuboresha matibabu sio tu Tanzania hata nchi za Afrika ndio maana leo hapa kuna wataalamu kutoka mataifa mbalimbali,”amesisitiza.

Mtaalamu wa afya kutoka nchini Uganda
Dk Zamzam kaberuka amesema anamatarajio ya kupata maarifa zaidi kutoka hapo na anatarajia kwenda kuwafundisha wataalamu wengine nchini kwako.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button