MTANDAO: WATUMIAJI wa dawa za maumivu katika mapishi hususani katika kulainishia kitoweo cha nyama, wapo hatarini kuugua magonjwa ya moyo, ini na figo.
Taasisi ya @elimu_ya_afya iliyo chini ya @wizara_afyatz imeeleza madhara hayo ikijibu chapisho la Mbunge wa Kigamboni @faustine_ndugulile juu ya taarifa za kuogofya kuhusu baadhi ya mama lishe kutumia dawa za kupunguza maumivu katika kuivisha na kulainisha kitoweo hususani nyama ya utumbo.
“Jambo hili ni hatari kiafya kwani
dawa hizi zinapopashwa moto
hutoa kemikali inayoitwa Amino, inapomeng’enywa na mwili huleta madhara,” imeeleza taarifa ya @elimu_ya_afya
Dk Ndugulile ni daktari kitaaluma, kupitia chapisho lake mtandaoni hakusita kugusia juu ya hatari ya matumizi ya dawa hizo zikichomwa au kuchemshwa.
“Athari ya dawa hizi zinapopikwa ni
kubwa, ikiwa ni pamoja na kuathiri figo, ini na moyo. Elimu kwa jamii inahitajika kwenye jambo
hili.
Nayo, Wizara ya Afya kupitia @elimu_ya_afya inaendelea kutoa wito kwa waandaji wa vyakula kuzingatia
maandalizi yanayojali afya ya
watanzania. #mtuniafya –