Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, leo Mei 21 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamula katika ofisi za Mkuu huyo wa Mkoa.
Katika ziara hiyo, Waziri Ulega atakagua miradi ya kimkakati inayotekelezwa Mkoani humo ikiwemo barabara ya mzunguko wa nje (Outer Ring Road) pamoja na Kiwanja che Ndege cha Kimataifa cha Msalato. (Picha na Wizara ya Ujenzi)