Ummy afafanua hatari kula matunda mchanganyiko

WAZIRI wa Afya ,Ummy Mwalimu ameonya ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza ifikapo 2030 huku akitahadharisha kuwa mtindo mbaya wa maisha ikiwemo ulaji usiofaa umekuwa sababu kubwa ya magonjwa hayo.

Ummy alisema ulaji wa matunda mchanganyiko ni sababu hatari kwa ugonjwa wa kisukari na kuwataka watu kuacha kuchanganya matunda wakati wa ulaji ambapo mtu anatakiwa kula tunda moja tu na baada ya nusu ya saa moja kula lingine.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya uelimisha ya magonjwa yasiyoambukiza ambapo pia amezindua mwangozo wa mtindo wa maisha na magonjwa yasiyoambukiza,mwongozo wa selimundu na vifaa vya kupima aliwasisitiza wataalmu kutoa elimu sahihi ya lishe inayofaa.

“Kuna mtindo wa kula matunda mengi kwa wakati mmoja tunadhani ndio mtindo bora hii haitakiwi kama unakula chungwa kula chungwa baada ya nusu saa kula lingine,lakini unaweka parachichi, embe,chungwa,tikiti maji ,papai,ndizi.

Ameongeza “Wataaamu naomba hili jambo msisitize tuwahamasishe wanaoandaa matunda matunda saba yanaongeza sukari nyingi tunafikiri ni afya kumbe unaenda kutengeneza sukari nyingi na kuna juisi wataalamu wanashauri kula juisi badala ya tunda na kama umatengeneza tumia tunda moja halafu usiongeze sukari.

Ummy amesema sasa nchi inashuhudia ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza hususan shinikizo la juu la damu,kisukari,saratani na zingin

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Seleman
Seleman
1 month ago

Mheshimiwa umeongea vizuri sana lakini kuna suala jingine linapaswa kutolewa ufafanuzi kitalaam na kiafya limekaaje? Ukienda kwenye masoko yetu kuna kitu kinaitwa chachandu mara nyingi hutumika katika kuongeza radha kwenye chakula kama samaki, nyama na vyakula vingine, chachandu hutengenezwa kwa mchanganyiko wa pilipili, nyanya, mbilimbi na aina zingine za viungo, chachandu huapatikana baada ya kuchanganya viungo kadhaa, kwa mantiki hiyo, naomba ofisi yako ifanye utafiti au ufuatiliaje wa chachandu kwa kuwa mara nyingi zinatengenezwa kienyeji. Hata hivyo, kufuatia ufafanuzi wako kuhusu ulaji wa matunda mchanganyiko kwamba unachangia katika kuongeza au kusababisha kisukari, je, mchanganyiko unaotumika kutengeneza chachandu katika masoko na maeneo mbalimbali nchini haziwezi kuwa chanzo cha magonjwa kwa binadamu? Lakini chachandu ninazozungumzia hapa ni pamoja na zinazoandaliwa na kufanyiwa packaging na wachakataji mbalimbali nchini Tanzania na baadae kupelekwa madukani.

Edward Alex Mkwelele
Edward Alex Mkwelele
1 month ago

Nafikiri ukila kupita kiasi

Research Doses
Research Doses
1 month ago

Habari hii inawezekana imepotoshwa. Matunda mchanganyiko ni muhimu sana. Utafiti unaonesha hatuli matunda na mboga vya kutosha. Pia sio kila tunda lina sukari na matunda ni bora kuliko juisi.

Back to top button
3
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x