Ummy akabidhi boti 2 wavuvi Tanga

MBUNGE wa Tanga Mjini na Waziri wa Afya  Ummy Mwalimu, leo  amekabidhi boti mbili zenye thamani ya Sh Mil 49 kwa vikundi vya uvuvi, mwani na majongoo bahari vyilivyopo Mtaa wa Mchukuuni, Kata ya Tangasisi mkoani Tanga.

Akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi boti hizo zenye thamani ya shilingi milioni 24. 5 kila moja sawa, ambazo  zimetolewa na taasisi ya Botna Foundation, amewataka  wana vikundi hao wa Mchukuuni kutumia boti hizo kuinua kipato chao na sio kutumia kwa matumizi ambayo hayajakusudiwa.

Akiwasilisha taarifa ya vikundi hivyo, Abdallah Mtondoo alimshukuru Waziri Ummy kwa kufanyia kazi maombi yao kwa haraka na hadi kupata boti hizo zitakazowasaidia kuinua kipato chao.

Advertisement

5 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *