GENEVA, Uswisi: ULAJI wa vyakula kwa kupunguza matumizi ya chumvi, sukari na mafuta husaidia kupunguza magonjwa yasiyoambukiza.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa taarifa hiyo leo Mei 27, 2024 baada ya matembezi maalum yajulikanayo kama ‘Walk the Talk, the health for all challenges’ yaliyoandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kila mwaka wakati wa mkutano wa mwaka wa ‘World Health Assembly (WHA)’ nchini Uswisi.
Waziri Ummy amesema lengo la matembezi hayo ni kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi ikiwa ni njia mojawapo ya kujilinda na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo Kisukari, Shinikizo la juu la damu pamoja na Saratani.
Soma pia: https://habarileo.co.tz/magonjwa-yasiyoambukiza-tishio-2030/
“Katika kuzingatia hilo, Tanzania imeanza kutekeleza kampeni hiyo ambapo hivi karibuni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, alizindua utaratibu wa kufanya mazoezi kwa wakazi wa Dar es Salaam ambapo ameruhusu kufungwa kwa barabara inayopitia daraja la Tanzanite ili itumike na wananchi kufanya mazoezi kuanzi saa 12:00 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi,” amesema Waziri Ummy.
Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7d5-DwNQvL/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==