Ummy ataja sababu kubwa ongezeko magonjwa ya moyo

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu ametaja sababu kubwa za kuongezeka kwa magonjwa ya moyo nchi huku akiwataka wananchi kuchukua hatua za haraka ili kuepuka gharama kubwa za matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema shinikizo la juu la damu na ugonjwa wa kisukari ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya moyo,figo na kiharusi.

Ameainisha kuwa takwimu zinaonesha ongezeko la wagonjwa wenye tatizo la moyo na shinikizo la juu la damu sasa ni asilimia 9.4 ambapo mwaka 2017 kulikuwa wagonjwa milioni 2.5 na mwaka 2022 wameongezeka mpaka milioni 3.4.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani iliyofanyika katika Hospitali ya Dar Group, Ummy amesema taarifa za ufuatiliaji wa magonjwa yasiyoambukiza mfano kisukari, shinikizo la juu la damu na saratani imeongezeka kutoka asilimia 1 mwaka 1980 hadi asilimia 9 mwaka 2020.

Waziri Ummy amebainisha kuwa utafiti mpya walioufanya taarifa zinaonesha katika kila watanzania 100 kuanzia miaka 15 ni watu 12 wanatatizo la kisukari na 25 wanatatizo la shinikizo la juu la damu ambapo ni mzigo mkubwa wa gharama.

“Kama Daktari akikwambia tumia dawa tafadhali tumia dawa kwani itakupeleka kupata kiharusi ,changamoto za figo na sasa kuna watanzania wengi wanasafisha figo kama jamii tuchukue hatua kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa ,kuhakikisha kupunguza matumizi ya chumvi,sukari ,mafuta kupita kiasi,”amesisitiza Waziri Ummy.

Aidha ameekeza kuwa takwimu zilizopo ni kuwa watanzania asilimia tatu wanatumia kiasi cha wastani wa kutosha wa matunda na mbogamboga huku asilimia kubwa wakiwa hawazingatii ulaji unaofaa.

“Hatuna shida ya vitu hivyo mbogamboga na matunda tunavyo elimu inahitajika hatutakiwi kuivisha sana mboga za majani na tunapaswa kufanya mazoezi angalau dakika 150 kwa wiki dakika 30 kwa siku.

Habari Zifananazo

Back to top button