Ummy atoa siku 7 kupata ripoti kifo cha mjamzito na kichanga

TANGA: Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa maelekezo kwa Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC) kuhakikisha ndani ya siku 7 wamempelekea taarifa ya tukio la kifo cha mjamzito na kichanga chake kilichotokea  Novemba 11 ,2023 mkoani Tanga.

Amesema, tayari hatua za awali zimeshachukuliwa ikiwemo ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba kutuma timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa inayojumuisha madaktari bingwa wawili akiwemo daktari bingwa wa wanawake na uzazi na daktari bingwa wa huduma za usingizi ili kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

“Hatua nyingine iliyochukuliwa baada ya tukio hilo ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kuwasimamisha kazi watumishi watatu walioshiriki kumpatia huduma mama huyo tangu alipopokelewa kituoni hadi umauti ulipomkuta ili kupisha uchunguzi wa tukio hili baya na lisilopaswa kuvumiliwa.” Amesema Waziri Ummy

Pia Waziri Ummy amewahakikishia Watanzania kuwa baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi, kila mtumishi aliyehusika atachukuliwa hatua kali za kitaaluma, kiutumishi na kijinai ikiwemo kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kijinai pale itakapothibitika.

Waziri Ummy ametoa pole kwa familia iliyoguswa na msiba huu na ameahidi kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya itaendelea kusimamia ubora wa huduma za afya ili kufikia matarajio ya wananchi wote.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
17 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions
.
.
.
On This Website……………..> > http://remarkableincome09.blogspot.com

Scholarship ya Mwanadamu mwenye
Scholarship ya Mwanadamu mwenye
16 days ago

Scholarship ya Mwanadamu mwenye akili ya ‘Kinyonga mdogo zaidi duniani’ aliyegundulika Tanzania

Kinyonga kwa jina Brookesia urefu wake ni milimita 13.5

Wanasayansi wanaamini kuwa wamebaini kinyonga mdogo zaidi duniani ambaye ukubwa wake ni sawa na mbegu.

Vinyonga hao wawili ilibainika nchini Madagasca na timu ya sayanasi ya Ujerumani na Madagasca.

Kinyonga wa kiume aliyepewa jina la Brookesia urefu wake ni milimita 13.5.
Na kinyonga huyo anakuwa mdogo zaidi kati ya spishi karibu 11,500 za vinyonga, kulingana na rekodi ya hifadhi ya wanyama ya taifa ya Bavaria katika mjini mkuu wa Munich.

Urefu wake kutoka juu hadi chini ni milimita 22.
Kinyonga wa kike ni mkubwa kidogo takribani milimita 29, taasisi hiyo imesema, ikiongeza kwamba aina nyingine bado hazijapatikana, licha ya kwamba “juhudi zimekuwa zikiendelea”.

“Kinyonga huyo mpya aliyepatikana kaskazini mwa Madagascar eneo la msitu linalopokea mvua kubwa, huenda yuko katika hatari ya kutoweka,” kulingana na jarida la wanasayansi.

Oliver Hawlitschek, mwanasayansi wa kituo historia huko Hamburg, alisema: “Kwa bahati mbaya eneo alilokuwa akiishi mjusi huyo lilianza kuingiliwa na binadamu lakini likaanza kulindwa hivi karibuni, kwahiyo anawezaa kunusurika.”

Watafiti walibaini kwamba kinyonga huyo alikuwa anatafuta mchwa katika msitu wenye mvua kubwa na kujificha dhidi ya wanyama wala nyama usiku kwenye nyasi.
Katika msitu ambao mjusi Brookesia alipatikana umepakana na misitu mingine kaskazini mwa kisiwa, walisema.

Katika ripoti yao, wanasayansi wamependekeza kuwa kinyonga huyo aorodheshwe kama mnyama aliye hatarini katika orodha ya Shirika la IUCN, linalochunguza hali ya maelfu ya jamii za wanyama kumsaidia kumlinda na makazi yake.

Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x