Ummy kushiriki kongamano la usalama barabarani

MTWARA: WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu  anatarajiwa kushiriki katika kongamano la usalama barabarani ambalo litafanyika mkoani Mtwara Oktoba 13, mwaka huu.

Kongamano hilo limeandaliwa na mabalozi wa Usalama Barabarani Tanzania (RSA) wakishirikiana na uongozi wa Kiwanda cha Dangote mkoani Mtwara kwa lengo kuhabarisha umma juu ya usalama barabarani.

Pia ni sehemu ya matukio mbalimbali ya usalama barabarani ambayo yameandaliwa na RSA ili kuadhimisha wiki ya mabalozi wa Usalama Barabarani Tanzania ambayo imeanza kuadhimishwa kitaifa mkoani hapa Oktoba 2, 2023.

Akiongea kwa niaba ya Mkurungezi wa RSA, Mwenyekiti wa Usalama Barabarani Mkoa wa Mtwara Nassoro Mansour amesema kongamano hilo litafanyika katika Kiwanda cha Dangote ambapo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu atakuwa mgeni Rasmi.

“Tumemualika mgeni Rasmi Waziri wa Afya kwa sababu sasa hivi suala la ajali barabarani limekuwa gonjwa kati ya yale magonjwa makuu kumi na tatu yanayomaliza watu wetu ulimwenguni,” amesema.

Mwenyekiti wa Bodi ya RSA Mohammed Kapinga amesema kongamano hilo litahudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo TANROADS, TARURA, zima moto, Wizara ya Ujenzi na Latra.

Watu wengine watakaoshiriki ni madereva, waendesha baiskeli na pikipiki (bodaboda), vikundi vya mazoezi, na watembea kwa miguu.

 

Habari Zifananazo

8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button