Ummy Mwalimu: Watu 32,000 huambukizwa VVU kwa mwaka

Watu 88 huambukizwa VVU kwa siku moja

TANGA: Takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu 32,000 hupata maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi nchini huku vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 wakiwa kwenye hatari zaidi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu Jijini Tanga wakati wa ufungaji wa kampeni ya jikubali iliyolenga kutoa elimu ya Ukimwi Kwa wanafunzi wa shule za sekondari kwenye mikoa minne nchini .

Amesema kuwa takwimu hizo zinaonyesha kuwa kwa siku moja takribani 88 hupata maambukizi mapya ya ugonjwa wa ukimwi hapa nchini.

“Kilichoshtua zaidi inaonyesha katika vijana 100 wenye umri wa miaka kati ya 15 hadi 24 vijana 67 wanapata maambukizi mpya hivyo kama Wizara tukaona tuje na kampeni hii Ili kuwasaidia vijana waweze kujilinda dhidi ya ugonjwa huo”amesema Waziri Ummy.

Nae Mratibu wa Programu ya Jikubali Catherine Johakim amesema kuwa kampeni hiyo imefanikiwa kuwafikia vijana waliopo mashuleni 10,2000 walioko kwenye Halmashauri 17 zilizopo kwenye mikoa minne hapa nchini.

“Wanafunzi hao wamepatiwa elimu ya kujiepusha na mimba za utotoni sambamba na magonjwa ya ngono ikiwemo maambukizi ya virus vya ukimwi”amesema Catherine.

Habari Zifananazo

Back to top button