Una ugonjwa wa kusahau? Tumia kahawa hii

UNAPOTEZA kumbukumbu na unahisi uwezo wako wa kufiri ni mdogo? Uwezo wa kufanya kazi unapungua kila siku ukiwa kazini, vipi hayo yakitokea bossi anasema nini juu yako?
Basi taarifa ikufikie kuwa huo ni ugonjwa kitaalamu unaitwa ‘Dementia’ sasa ili kuepukana nao utafiti uliofanywa na Profesa Mariapina D’Onofrio kutoka Chuo Kikuu cha Modena na Reggio Emilia, Verona nchini Italia umeshauri yafuatayo.
Katika utafiti wake, Prof Mariapina ametaja kinywaji ambacho maelfu ya watu hufurahia na kinaweza kusaidia kupunguza hatari ya ugonjwa wa shida ya akili.
ESPRESSO
Ametaja kinywaji cha Espresso: Hii ni aina ya kahawa yenye mchanganyiko wa vitu mbalimbali ambavyo inapatikana nchini Italia.
Prof Mariapina ameshauri kila siku kunywa kikombe kimoja kwa kiasi kikubwa kunaweza kupunguza hatari ya kupata shida ya akili, haswa ugonjwa wa Alzheimer’s.
Utafiti huo unaonesha kinywaji hicho kina uwezo wa kukabiliana na uundaji wa protini za tau, ambazo zinajulikana kwa kujilimbikiza katika akili za watu wenye magonjwa ya neurodegenerative.
Utafiti huo unaeleza watu wenye afya njema, protini za tau huchukua jukumu muhimu katika kuleta uthabiti wa miundo ya ubongo lakini kwa wale walio na magonjwa ya mfumo wa neva, protini hizi zinaweza kukusanyika pamoja na kuwa ‘nyuzi’ hatari zinazovuruga utendaji kazi wa neva. Hii inaweza kusababisha uharibifu wa utambuzi tabia ya shida ya akili.
Kama sehemu ya utafiti, majaribio kadhaa yalifanywa na kugundua kuwa espresso inapingana kikamilifu na malezi ya nyuzi hizi. Utafiti pia ulibainisha mtazamo wa kijiografia kwa matokeo.
Utafiti huo pia umebaini kuwa karibu asilimia 96 ya Waitaliano hutumia espresso kila siku, ambayo inaonesha tabia ya lishe ambayo inaweza kuchangia kiwango cha chini cha ugonjwa wa shida ya akili katika maeneo fulani.
Espresso inaweza kuzuia mkusanyiko wa protini ya tau – mchakato ambao unaaminika kuhusika katika kuanza kwa ugonjwa wa Alzheimer.
[12:17, 10/08/2023] @Mrtarafa: SIMBA SC mpaka sasa haijawasilisha vibali vya wachezaji wa kigeni, kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka (TFF) iliyotolewa leo.
–
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano, TFF imesema Singida FG pia haijafanya hivyo.
–
TFF imezikumbusha klabu hizo kuwa wachezaji ambao hawajapata vibali hivyo hawataruhusiwa kucheza mchezo wa leo wa Ngao ya Jamii.