Usafi sasa kila Jumamosi

DAR ES SALAAM: MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema kuwa zoezi la Usafi katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ni kila jumamosi, lengo likiwa ni kufanya jiji kuendelea kuwa katika hali ya usafi.

Mpogolo ameeleza hayo wakati wa zoezi maalum la usafi lililofanyika leo siku ya jumamosi Februari Mosi, 2025 kwa Kanda namba 1 na 2 za Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kuanzia eneo la Kamata, Mtaa wa Gerezani kupitia barabara ya Sokoine, Kivukoni front, Luthuli, barabara ya Barack obama kuelekea fukwe za Dengue.

Usafi huo umefanyika kuanzia kuanzia saa 12:30 Asubuhi mpaka saa 4:00 Asubuhi.

“Tumekubaliana na wenzangu ili kulifanya Jiji letu kuendeleza kuwa safi na beach yetu hii kuendelea kuwa safi, Zoezi hili la usafi kwa wilaya ya llala ni la kila siku lakini kukutana kwa pamoja ni kila jumamosi.”

Pia, Mpogolo ametoa wito kwa Wananchi, taasisi na wadau mbalimbali wa mazingira kujitokeza katika mazoezi ya endelevu ili khakikisha jiji letu linaendelea kuwa safi kwa jitihada za pamoja na kwa vitendo.

Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, amesema ofisi yake itaendelea kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya
kufanyia usafi katika mazoezi hayo kwa kushirikiana na Wakandarasi wa usafi wanaofanya kazi ndani ya jiji la DSM.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button