Usalama usafiri wa anga kuimarisha uchumi

DAR ES SALAAM: MAMLAKA ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imesema usalama wa anga na viwanja vya ndege uliopo kwa sasa umechangia kuongeza kukua kwa kiasi kikubwa cha uchumi wa nchi kutokana na kuimarishwa kwa usalama huo.

Mkuu wa Udhibiti wa Viwango Viwanja vya Ndege Tanzania, Vedastus Fabian kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo,  Abdul Ramadhani Mombokaleo katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Utamaduni wa Usalama wa Usafiri wa Anga ambapo imeanza leo hadi Oktoba 25.

Advertisement

Aidha Vedastus amesema usalama ukiwa dhabiti kwenye viwanja na anga  taifa litapata tija kwenye nyanja ya uwekezaji hivyo na nchi kuaminika kwa wageni wanaoingia na wanaotoka ndani na nje ya nchi.

“Usalama wa usafiri wa anga unasafirisha  bidhaa, wawekezaji ,viongozi wetu, watalii na watu wengine  hivyo usalama wa usafiri wa anga unapoimarika watalii wengi watakuja wakiwa na uhakika tulienda Tanzania tunawasili salama  na tunaondoka salama,”

“Kwa hiyo itachangia kukuza uchumi na pamoja na ulinzi wa watu wanatumia viwanja vyetu pamoja na mali zao viongozi wetu pia wanalindwa wa ndani ya nchi na nje ya nchi usalama ukiwa thabiti hawa wote tunahakikisha wapo salama,” amesema Vedastus.

Jackline Ngoda mfanyakazi wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) amesema  wao kama wafanyakazi usalama wa anga ni kipaumbele chao ndio maana huduma  ubora na ufanisi kwenye viwanja vya tanzania ni mkubwa.